Wanajeshi wa Mali wametangaza kuumiliki mkoa wa Bamako na kuiteka ikulu ya Raisi wa Jamhuri wa nchi hiyo, nao wamesema kuwa kuiteka ikulu hiyo imetokea baada ya mapigano makali na wanajeshi wanaolinda ikulu hiyo na kufanikiwa kuwakamata baadhi ya mawaziri miungoni mwao waziri wa mambo ya nje na waziri wa Ardhi.Ama taarifa hizi Mpaka sasa hazija tangazwa rasmi na Serikali ya Jamhuri ya Mali. Katika hali hiyo imeelezwa kuwa Raisi wa Mali mpaka sasa hajarudi ikulu. Kwamujibu wa ripoti hii inaarifiwa kuwa mapigano yalianza usiku wa jumaa nne ambako kulitokea mapambano makali baina ya jeshi linalo linda ikulu hiyo na wanapinduzi hao.
21 Machi 2012 - 19:30
Msimbo wa Habari: 304045
Watu wenye silaha nchini Mali wametangaza kuimiliki ikulu na kuipindua Serikali ya nchi hiyo.